728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    GOOD NEWS KWA MASHABIKI WA CHELSEA:KURT ZOUMA IS BACK

    Etienne,Ufaransa.

    AMERUDI!!HALI ya mlinzi wa Chelsea aliyekuwa majeruhi Mfaransa Kurt Zouma imezidi kuimarika baada ya staa huyo wa zamani wa St.Etienne kuanza kufanya mazoezi ya kukimbia na kuchezea mpira tayari kwa mshikemshike wa msimu mpya wa Ligi Kuu England.

    Zouma,22,ambaye kwa sasa yuko nyumbani kwao Ufaransa akiuguza jeraha la goti alilolipata mwezi Februari katika mchezo wa Ligi Kuu England ulioisha kwa klabu yake ya Chelsea kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Manchester
    United huko Stamford Bridge ameweka Video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa katika mazoezi makali.

    Video hiyo yenye Ujumbe unaosomeka  “Step by Step” yaani hatua kwa hatua inaashiria Zouma atarejea dimbani mapema kuliko ilivyodhaniwa hapo awali kwamba angekuwa nje kwa zaidi ya miezi sita.

    Kabla ya kupata jeraha hilo baya lililokatisha ndoto yake ya kucheza michuano ya Ulaya (Euro) kwa mara ya kwanza,Zouma alikuwa tayari amefanikiwa kuichezea Chelsea jumla ya 32 katika michuano yote kufuatia kumpokonya namba mlinzi Gary Cahill.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GOOD NEWS KWA MASHABIKI WA CHELSEA:KURT ZOUMA IS BACK Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top