728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 31, 2016

    UMEISIKIA HII YA WACHEZAJI 11 WA TIMU MOJA KUUGUA KIPINDUPINDU?

    Morogoro,Tanzania.

     Klabu ya Muheza United FC ya Tanga imeshindwa kuendelea na michezo ya Ligi ya Mabingwa wa
    Mikoa baada ya wachezaji wake 11 kuugua ugonjwa wa kipindupindu na kulazwa katika kituo cha afya cha Sabasaba, Manispaa ya Morogoro.

    Msimamizi wa kituo cha Morogoro kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Charles Ndagala alisema mchezo kati ya Stend FC ya Pwani na Muheza United FC uliopangwa kufanyika saa
    nane mchana umesogezwa mbele kufuatia wachezaji 11 wa Muheza United kuugua kipindupindu.

    Ndagala alisema kutokana na dharura hiyo mchezo huo utapangwa siku nyingine hadi afya za wachezaji hao zitakapotengemaa.

    “Mgonjwa wa kwanza aligundulika majira ya saa nane usiku na wengine
    wanne kukimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro na walipimwa na
    kugundulika kuwa wanaugua kipindupinduu,” alisema Ndagala.

    Kocha wa Muheza United, John ‘King’ Kibwana aliwataja wachezaji
    waliolazwa kuwa ni Iddi Bohero,Ramadhan Rajabu, Jerd Stephen, Nirmo Rashid Sendeka, Abdul Mashaka, Pima Omari, Athman Mwandani, Robert
    Newa na Iddi Kadabla.
    Ofisa Afya wa Manispaa ya Morogoro,Dk Gabriel Malissa alisema waliwapokea wagonjwa 11 na kuwalaza katika kituo cha afya Sabasaba na hali
    zao zinaendelea vizuri.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UMEISIKIA HII YA WACHEZAJI 11 WA TIMU MOJA KUUGUA KIPINDUPINDU? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top