Victor Wanyama.
Nairobi, Kenya.
Timu ya taifa ya soka ya Tanzania "Taifa Stars" leo jioni iitakuwa ugenini Moi Kasarani kuvaana na timu ya taifa ya Kenya "Harambee Stars" katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Mchezo huo unaotambuliwa na FIFA na utakaochezeshwa na mwamuzi Brian Nsubuga toka Uganda ni maalumu kwa ajili ya kuziandaa timu hizo zinazokabiliwa na mechi za kufuzu michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Congo DR na Misri.
Katika mchezo huo ambao
utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Azam Tv kwa kushirikishikiana na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) saa 10:00 Kamili Jioni,Taifa Stars itawakosa washambuliaji wake mahiri Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wamebanwa na majukumu katika vilabu vyao.
Kenya wao wamepata afueni baada ya nahodha wao Victor Wanyama kupona majeraha yaliyokuwa yakimkabili na huenda akacheza mchezo wa leo.
0 comments:
Post a Comment