728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 29, 2016

    RASHFORD ALAMBA KANDARASI MPYA MAN UNITED,MSHAHARA JUU,BONASI JUU

    MANCHESTER, ENGLAND.


    Manchester United imempa mkataba/kandarasi mpya ya muda mrefu mshambuliaji wake kinda Marcus Rashford,18.

    Kandarasi hiyo mpya inayotarajiwa kutangazwa rasmi kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016 imedaiwa kuwa ni ya miaka minne na itamuwezesha Rashford kuvuna mshahara wa £20,000 kwa wiki pamoja na bonasi ya maana.

    Kwasasa Rashford ambaye ameifungia Manchester United mabao manane katika michezo 18 anavuna mshahara wa £1,500 kwa wiki na bonasi inayodaiwa kufikia £5,000.

    Mbali ya Rashford kinda mwingine anayetarajia kuingia kandarasi mpya ni mlinzi wa kushoto Cameron Borthwick-Jackson,19.

    Manchester United imeamua kuwapa kandarasi mpya nyota hao ili kuondoa uwezekana wa kuwapoteza kwa vilabu vingine.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASHFORD ALAMBA KANDARASI MPYA MAN UNITED,MSHAHARA JUU,BONASI JUU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top