London,England.
Arsenal imezindua jezi zake mpya itakazozitumia katika msimu wa 2016-17.
Jezi hizo nyekundu/nyeusi na blue zilizotengenezwa na kampuni ya Puma hazina tofauti sana na jezi zilizozoeleka isipokuwa kuna tofauti ndogo katika sura/muonekano wa jezi ya juu na bukta.
Katika jezi ya juu kuna mstari umepita katikati kuanzia shingoni na kuishia kiunoni.Bukta ina mstari mpana upande wa mapajani kwa nje.
Ukizitazama jezi hizo utagundua kuwa Puma wamefanya kazi nzuri.Jezi zinavutia sana lakini tatizo liko kwenye bei.
Kwa mashabiki:Jezi ya mikono mifupi inauzwa £55 (Tsh 137,500) huku jezi ya mikono mirefu ikiuzwa kwa £60 (Tsh 150,000)
Jezi halisi inayovaliwa na wachezaji kwenye mechi (The authentic match shirt) itakuwa ikiuzwa kwa £100 (Tsh 250,000)
Wakati huohup Arsenal imetanabaisha kuwa nyota wake Mchile Alexis Sanchez ameachana na jezi Namba 17 na sasa atakuwa akivaa jezi Namba 7 iliyokuwa ikivaliwa na Tomas Rosicky.Uzinduzi rasmi utafanyika Juni 3 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment