Timu za taifa za soka za Tanzania Taifa Stars na Kenya Harambee Stars jioni ya leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.
Katika mchezo huo uliokuwa maalumu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON mapema mwezi ujao,Taifa Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 33 kupitia kwa mshambuliaji wake Elius Maguli.Maguli alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya mlinzi wa kulia Juma Abdul
Baada ya kuingia kwa bao hilo Harambee Stars ilikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 38 kupitia kwa nahodha wake Victor Ngubi Wanyama.Wanyama alifungia bao hilo kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Shiza Kichuya kumwangusha ndani ya boksi Ayub Timbe Masika.
Mpaka kipyenga cha mwamuzi Brian Nsubuga kutoka Uganda kinapulizwa kuashiria mchezo umekwisha matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment