Paris,Ufaransa.
Beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane,23 ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitachoshiriki michuano ijayo ya Euro itayoanza mwezi June kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.
Pia nyota huyo wa klabu ya soka ya Real Madrid ataukosa mchezo wa fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya utakaopigwa Mei 28 kati ya timu yake na Atletico Madrid huko San Siro,Milan-Italia.
Varane anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu mpaka nne na nafasi yake kwenye kikosi cha taifa imechukuliwa na beki Adil Rami, mwenye umri wa miaka 30 anayeichezea timu ya Sevilla ya nchini
Hispania.
Rami ambaye hivi karibuni ameisaidia Sevilla kutwaa ubingwa wa Europa Ligi,hakuwa katika kikosi cha akiba/standby cha Kocha Didier Deschamps na hajawahi kuichezea Ufaransa tangu June mwaka 2013 alipojumuishwa kwa mara ya mwisho.
Varane anakuwa beki wa pili kuzikosa fainali za mwaka huu za Euro kutokana na majeruhi baada ya beki wa Chelsea Kurt Zouma
0 comments:
Post a Comment