Dar es Salaam,Tanzania.
FEDHA inaongea, baada ya kuifanyia Simba umafia kwa kuwasajili Hassan Ramadhan ‘Kessy’ na Juma Mahadhi sasa jeuri ya Yanga imehamia kwa Azam, baada ya kumnasa straika wa timu hiyo, Kipre Tchetche kwa dau la shilingi milioni 180.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani,Yanga tayari imemnasa Kipre kwa dau hilo la fedha na kumfunga Jangwani na mkataba wa miaka mitatu.
Inadaiwa kuwa kuondoka kwa kocha Stewart Hall katika klabu ya Azam kumewaumiza mastaa wengi wa kimataifa wa timu na ndiyo moja ya sababu kubwa za Kipre kuamua
kutimkia Jangwani.
Chanzo cha habari hizi kimemsema kuwa mbali na kumtimua Hall, Azam pia
imekuwa na mpango wa kutaka kumuondoka kwenye timu hiyo Kipre Bolou pacha wa Tchetche kitendo ambacho kilimuumiza staa huyo ambaye aliamua kutua Jangwani.
Yanga imekuwa ikifukuzia saini ya Kipre Tchetche kwa muda mrefu sasa na kati siku za karibuni inadaiwa kuwa staa huyo amekuwa akikutana kwa siri na baadhi ya viongozi wa miamba hiyo ya Jangwani.
“Unajua kwa nini Kipre hakucheza fainali ya Kombe la Shirikisho?” kilihoji chanzo cha habari hizi. “Kabla ya fainali walitakiwa wasitoke kambini, lakini yeye alitoka na kukutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kujadili masuala ya usajili.”
Inadaiwa kitendo cha kutoka kambini bila ruhusu ndiyo kilisababisha asipangwe kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo Yanga ilichukua ubingwa kwa kuichapa Azam kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa.
Licha, ya viongozi wa Yanga kuonekana kufanya siri sana ishu hii ya usajili wa Kipre,lakini chanzo cha habari hizi kimesema kuwa siku si nyingi kutoka sasa habari hizi ambazo zinatarajiwa kulishtua Taifa zitatangazwa rasmi.
Pamoja na Yanga kudaiwa kukamilisha usajili wa Kipre, staa huyo anadaiwa kuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja Azam na klabu yake hiyo imedai kuwa kama Yanga wanataka kumchukua basi wafuate utaratibu kwa kukaa nao mezani na kumalizana kwa sababu wao hawana nia ya kumzuia mchezaji kama anataka kujiunga na timu nyingine.
CHANZO:BINGWA
0 comments:
Post a Comment