Dar es salaam,Tanzania.
SHIRIKISHO la vyama vya soka nchini TFF limesema kuwa Tanzania haitaandaa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwaka 2016 kama ilivyokuwa imeripotiwa Awali.
Tamko hilo limetolewa leo na Rais wa Shirikisho hilo,Jamal Malinzi.Akiongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini leo Malinzi amesema hatua hiyo imetokana na Tanzania kukabiliwa na ratiba ngumu ya michuano mbalimbali ya Kimataifa kati ya mwezi Juni na Septemba.
Malinzi ameongeza kuwa suala la kuandaa michuano hiyo lilikuwa chini ya Zanzibar ambayo baadaye ilitangaza hivyo TFF ilitaka kulichukua jukumu hilo baada ya kuombwa na CECAFA lakini kwa sababu ya kubanwa na ratibu imeona ni vyema ikajitoa ili kutoa nafasi kwa Yanga SC na Taifa Stars kujiandaa na michezo iliyo mbele yao.
0 comments:
Post a Comment