728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 31, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO MEI 31,2016

    Breel Embolo

    Embolo:Tottenham imeripotiwa kuwa itamgeukia mshambuliaji wa FC Basel Mswisi Breel Embolo,19, ikiwa watashindwa jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Marseille Mbelgiji Michy Batshuayi,22.Embolo ameifungia Basel mabao 30 katika michezo 86.(Daily Telegraph)

    Alaba:Bayern Munich imekataa ofa ya €50m toka Real Madrid kwa ajili ya kumuuza beki wake wa kushoto Muaustria David Alaba,24.(AS)

    Bacca:West Ham imepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuripotiwa kutuma ofa ya £15m ili kumsajili mshambuliaji wa AC Milan Mcolombia Carlos Bacca.Bacca,29,ameifungia AC Milan mabao 18 msimu huu ataruhusiwa kuondoka San Siro kwa dau la £19m.(Gazette dello Sport)

    Toprak:Borussia Dortmund imeanza kumfukuzia beki wa Bayer Leverkusen,Omer Toprak ili kuziba nafasi ya Mats Hummels aliyetimkia Bayern Munich.(Bild)

    Asamoah:Meneja Mpya wa Chelsea Muitaliano Antonio ameendelea kuhusishwa na mpango wa kutaka kumsajili kiraka wa Juventus Mghana Kwadwo Asamoah na tayari ameripotiwa kutenga kitita cha €20m ili kumnasa staa huyo wa zamani wa Udinese.(Gazzetta Dello Sport)

    Zielinski:Liverpool huenda ikashindwa kumnasa winga wa Empoli Mpoland,Piotr Zielinski,22,baada ya Napoli kudaiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili nyota huyo ambaye atakuwa huru kuanzia Julai 1.(La
    Gazzetta dello Sport)

    Robben: Besiktas inataka kumsajili winga wa Bayern Munich Mdachi Arjen Robben,31, ili kuchukua nafasi ya winga wake Gokhan Tore anajiandaa kuhamia West Ham.(Mynet)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO MEI 31,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top