728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 24, 2016

    YANGA JEURI BHANA YAWAAMBIA WACHEZAJI CHAPA AZAM KESHO TUWAJAZE MAPESA.

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Kutokana na kiwango bora cha Yanga msimu huu, mabosi wa timu hiyo
    wameamua kutangaza neema kwa wachezaji kwa ahadi ya kugawana fedha
    zote za ubingwa wa Kombe la FA ikifanikiwa kuutwaa.

    Yanga itacheza na Azam katika fainali ya
    Kombe la FA kesho Jumatano na bingwa wa mashindano hayo ataondoka na kitita cha Sh 50 milioni. Tayari viongozi wa Yanga wamewaambia wachezaji wao zitakuwa za kwao.

    Kutokana na hali hiyo wachezaji wameonekana kupata hamasa kuelekea
    mchezo huo na kiraka Mbuyu Twite amesema kuwa wataweka heshima kama watafanikiwa kuifunga Azam.

    “Tumefanya kazi kubwa
    Angola na sasa tunatakiwa kumalizia kazi hii kwa Azam, nadhani hapo ndipo
    tutakuwa tumeweka rekodi zetu vizuri.

    “Mpaka sasa hatufahamu Azam huwa wanawezaje kutuzuia, lakini tutapambana katika mchezo huu tuwafunge, ni jambo linalowezekana,” alisema Twite.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA JEURI BHANA YAWAAMBIA WACHEZAJI CHAPA AZAM KESHO TUWAJAZE MAPESA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top