Kabasele
Brussels, Ubelgiji.
Jinamizi la majeruhi limeendelea kuikumba kambi ya timu ya taifa ya Ubelgiji inayojiandaa na michuano ya Ulaya [Euro 2016] baada ya walinzi wake wawili Nicolas Lombaerts na Dedryck Boyata kulazimika kuondolewa kikosini kutokana na kuwa majeruhi.
Lombaerts ambaye ni mlinzi wa kutumainiwa wa klabu ya Zenit St Petersburg ameondolewa kutokana na kusumbuliwa na misuli huku Boyata anayecheza Celtic yeye ameondolewa kutokana na kupata jeraha ambalo haliwezi kupona kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Hali hiyo imemfanya Kocha Mkuu wa kikosi hicho Marc Wilmots kumuita kwa mara ya kwanza kikosini mlinzi Christian Kabasele wa Klabu ya KRC Genk inayochezewa na Mtanzania Mbwana Samatta ili kuja kuziba nafasi hizo.
Kuumia kwa Lombaerts na Boyata,ni pigo kubwa kwa Ubelgiji kwani kabla ya hapo ilikuwa imeshampoteza nahodha wake Vincent Kompany kutokana na kuumia misuli huku pia ikimpoteza Bjorn Engels anayesumbuliwa na goti.
Ubelgiji iko kundi E la Euro 2016 na itacheza mchezo wake wa kwanza kwa kuvaana na Italia Juni 13 huko Lyon.
0 comments:
Post a Comment