Barcelona,Hispania.
UJANJA mwingi mbele kiza.Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuelezea hiki ilichotaka kukifanya klabu ya FC Barcelona.
Klabu ya FC Barcelona imeangukia pua katika mbio zake za kumuwania mlinzi wa Atletico Nacional ya Colombia, Davinson Sanchez.
Habari iko hivi!!Licha ya FC Barcelona na Atletico Nacional kufikia makubaliano ya kuuziana mlinzi huyo kwa ada ya €3.5m (£2.8m) usajili huo umekwama baada ya Davinson,19 kugundua kuwa lengo la FC Barcelona lilikuwa ni kumfanyisha mazoezi katika kikosi cha wakubwa chenye Messi,Neymar Jr na kisha imtumie katika kikosi cha pili cha Barcelona B kinachoshiriki Ligi daraja la tatu.
Akitoa taarifa hizo wakala wa Davinson,aitwaye Nestor Villarreal,amesema
“ Davinson amebadili uamuzi baada ya kugundua kuwa FC Barcelona ilitaka kumtumia katika kikosi chake cha pili cha Barcelona B kinachoshiriki Ligi daraja la tatu na siyo kile cha wakubwa kinachocheza Ligi ya La Liga.
"Hataki kucheza Ligi ya chini wakati kwasasa yuko Ligi ya juu.Ameamua kubaki Atletico Nacional na kuisaidia Klabu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya Copa Libertadores".
0 comments:
Post a Comment