Ewen Mackenzie akiwa na Kenny Cameron
Inverness,Scotland.
KILA mmoja wetu ana ndoto na ili itimie anahitaji kupambana kweli kweli.Unaweza ukastaajabu na usiiamini kabisa habari hii lakini ukweli unabaki kuwa kama ulivyo!!
Hivi karibuni Klabu ya Inverness Caledonian Thistle inayoshiriki Ligi Kuu ya Scotland iliondokewa na aliyekuwa Kocha wake Mkuu John Hughes.Mapema uongozi ukaanza kusaka Kocha mpya,Maombi yakaanza kuja.
Moja kati ya maombi hayo yalitoka kwa mtoto Ewen Mackenzie ambaye umri wake ni miaka 7 pekee tena akiwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi.
Katika barua iliyoandikwa kwa mkono,Ewen alijitambulisha kuwa yeye ni mwanafunzi,umri wake ni miaka 7 na kuwa anataka kuziba nafasi ya Hughes aliyetimka klabuni hapo.
Ewen akaelezea jinsi ambavyo atakuwa akimuomba ruhusa mwalimu wake ili awahi katika mazoezi mazoezini na mechi zote muhimu.
Uongozi wa Inverness Caledonian Thistle kupitia kwa mwenyekiti wake Kenny Cameron uliipokea na kuisoma barua hiyo na kisha kuijibu kuwa unashukuru kwa maombi hayo lakini hauwezi kumpa Kazi kwani ni mdogo sana na hana sifa zinazohitajika kwa sasa.
Azingatie masomo yake na labda siku moja atakuja kutimiza ndoto hiyo ya kuwa kocha.
0 comments:
Post a Comment