Madrid,Hispania.
Habari kutoka gazeti la Daily Star zinasema kuwa Kocha Mkuu wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone "El Cholo" amewapa mtihani mgumu mabosi wa kikosi hicho ambao kama wataufaulu basi ataendelea kubakia klabuni hapo.
Imedaiwa baada ya kuona FC Barcelona ikitwaa ubingwa wa La Liga na Real Madrid ikikifunga kikosi chake Jumamosi na kutwaa ubingwa wa Ulaya,Simeone ameumia sana na amewaambia mabosi wake wamletee wachezaji wakali watakaomfanya aweze kutwaa mataji vinginevyo wamwache aondoke zake.
Simeone anaamini kama angekuwa na mshambuliaji mkali kama Diego Costa basi angeweza kutwaa ubingwa wa La Liga ama ule wa Ulaya ambao ameukosa mara mbili kwa kufungwa na Real Madrid katika finali ya mwaka 2014 na 2016.
Diego Costa aliisaidia Atletico Madrid kutwaa taji la La Liga mwaka 2014 kabla ya kujiunga na Chelsea mwaka huohuo kwa ada ya £35.
0 comments:
Post a Comment