728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 24, 2016

    MISRI YATANGAZA 25 WA KUIVAA TAIFA STARS,ELNENY,SALAH WAMO

    CAIRO,MISRI.

    KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri Muargentina Hector Cuper leo ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachokuja Tanzania kucheza na Taifa Stars katika mchezo wa marudiano wa kundi G wa kuwania kufuzu fainali ya michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Gabon mwakani.

    Katika mchezo huo uliopangwa kuchezwa Juni 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam,Cuper amewaita kikosini kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny na winga wa Roma Mohamed Salah huku akimtema nahodha wa Ahly Hossam Ghaly kutokana na kuwa na ugomvi na benchi la ufundi.

    Misri inaongoza kundi G ikiwa imejikusanyia pointi saba baada ya kucheza michezo mitatu,nafasi ya pili inashikwa na Nigeria yenye pointi mbili nafasi ya tatu inashikwa na Taifa Stars yenye pointi moja.

    Ushindi au sare yoyote dhidi ya Taifa Stars Juni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam itaifanya Misri ifuzu AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.

    KIKOSI KAMILI

    Makipa: Essam El-Hadary (Wadi Degla),Sherif Ekrami (Ahly) and Ahmed El-Shennawy (Zamalek)

    Mabeki: Ahmed Fathi (Ahly), Mohamed Abdel-Shafy (Saudi Ahly), Hazem Emam
    (Zamalek), Ahmed Hegazy (Ahly), Rami Rabia (Ahly), Sabry Rahil (Ahly), Ali Gabr (Zamalek),Ayman Ashraf (Smouha), Hamada Tolba (Zamalek) and Karim Hafez (Omonia)

    Viungo: Abdullah El-Said (Ahly), Hossam Ashour (Ahly), Mohamed Elneny (Arsenal),Mohamed Salah (Roma), Mohamed Ibrahim (Zamalek), Tarek Hamed (Zamalek), Mohamed
    Hassan 'Trezeguet' (Anderlecht), Moemen Zakareya (Ahly) and Amr Warda (Panetolikos)

    Washambuliaji: Marwan Mohsen (Ismaily), Ahmed Hassan 'Kouka' (Braga) and Amr Gamal (Ahly)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MISRI YATANGAZA 25 WA KUIVAA TAIFA STARS,ELNENY,SALAH WAMO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top