Liverpool,England.
WAKATI vilabu vingine vya Ligi Kuu England vikiwa bado haijulikani ni lini vitaingia rasmi sokoni kusaka wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao,Liverpool yenyewe imekaribia kukamilisha usajili wa tatu.
Kutoka jijini Liverpool katika viunga vya Merseyside habari zinasema Kipa wa Mainz ya Ujerumani Loris Karius,22 tayari yuko Anfield na muda wowote kuanzia sasa ataanza kufanyiwa vipimo vya afya na mambo yakienda sawia atajiunga na Liverpool kwa ada ya Paundi milioni 4.7.Karius ameletwa kuja kuwapa changamoto zaidi Simon Mignolet na Adam Bogdan.
Kabla ya kujiunga na Mainz Karius alikuwa katika shule ya soka ya Manchester City kati ya mwaka 2009 na 2011 akifanikiwa kuvichezea vikosi vya vijana vya klabu hiyo vya U-18 na U-21.
Karius ambaye usajili wake umepangwa kutangazwa kesho Jumanne atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Kocha Jurgen Klopp baada ya Marko Grujic na Joel Matip.
Wachezaji wengine wanaowindwa na Klopp ili kuja kuipa makali Liverpool ni kiungo wa Bayern Munich Mjerumani Mario Gotze,Kiungo wa Borussia Monchengladbach Mahmoud Dahoud na mlinzi wa kushoto wa Leicester City Muingereza Ben Chilwell.
0 comments:
Post a Comment