Manchester, England.
Hatimaye klabu ya Manchester United rasmi leo imemtangaza Mreno Jose Mourinho kuwa kocha wake mkuu mpya.
Mourinho,53 amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuinoa miamba hiyo ya Old Trafford.Mkataba huo utakaofikia tamati mwaka 2019 pia umewekewa kipengele cha kurefushwa ikiwa pande zote mbili zitaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Mourinho ataiongoza Manchester United kucheza mchezo wake wa kwanza Ijumaa ya Julai 22 pale itakapovaana na Borussia Dortmund katika mchezo wa maandalizi ya msimu mpya utakaochezwa huko Shanghai,China.
Wakati huohuo habari zinasema Mourinho atamjumuisha kwenye benchi la ufundi msaidizi wake wa muda mrefu Rui Faria.
0 comments:
Post a Comment