728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    WACHEZAJI REAL MADRID KUJAZWA MANOTI WAKITWAA UCHAMPION WA LIGI YA MABINGWA ULAYA KESHO JUMAMOSI

    Madrid,Hispania.

    WASHINDWE WENYEWE!!Klabu ya Real Madrid imeahidi kuwapa wachezaji wake bonasi ya €600,000 ( Tsh,1230000000) kila mmoja ikiwa  wataifunga Atletico Madrid na kutwaa Uchampioni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho Jumamosi.

    Ahadi hiyo imekuja wakati Real Madrid ikiripotiwa kupania kuweka rekodi ya kutwaa  ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya 11 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1955.

    Bonasi hiyo ni zaidi ya ile ya €400,000 iliyotolewa mwaka 2014 kwa wachezaji wa miamba hiyo ya Santiago Bernabeu pale walipoibuka wababe baada ya kuichapa Atletico Madrid kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa huko Estadio da Luz,Lisbon-Ureno.

    Real Madrid na Atletico Madrid zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi katika mchezo wa Fainali utakaopigwa huko San Siro,Italia na mshindi atatia kibindoni kitita cha €120m.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WACHEZAJI REAL MADRID KUJAZWA MANOTI WAKITWAA UCHAMPION WA LIGI YA MABINGWA ULAYA KESHO JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top