Munich,Ujerumani.
Mario Götze amezima uvumi kuwa ataihama Bayern Munich na kuhamia Liverpool katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya kusisitiza kuwa atabaki Allianz Arena na kugombea namba katika kikosi cha kocha Mpya wa Klabu hiyo Muitaliano Carlo Ancelloti.
Katika kudhihirisha kuwa hana utani katika jambo hilo Gotze,23 ameripotiwa kumtupia virago wakala wake wa muda mrefu Volker Struth wa kampuni ya uwakala ya Sport Total Agency yenye makao yake makuu katika mji wa Cologne.
Sababu za kumtupia virago wakala huyo ni kwamba Gotze amemtuhumu Struth kuwa amekuwa akimchonganisha na Bayern Munich kwa kukosoa mambo mengi yanayofanywa na miamba hiyo ya Allianz Arena huku pia akilazimisha kumpeleka Liverpool.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema Götze atakuwa chini ya kampuni ya Uwakala ya ROGON Sports
Management Group ambayo pia inawawakilisha Roberto Firmino na Loris Karius.
0 comments:
Post a Comment