Manchester, England.
Antony Martial ndiye Usain Bolt wa Manchester United!!Ndivyo tunavyoweza kusema kwasasa kuhusu kijana huyo toka Ufaransa.
Wakati Usain Bolt akiendelea kutamba kwa kuvunja na kuweka rekodi katika mchezo wa riadha kwa kutimua mbio kwa kasi ya ajabu,Anthony Martial ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Manchester United aliyekuwa na kasi zaidi msimu ulioisha wa 2015-16.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Opta,Martial alikimbia kwa kasi ya Kilometa 35.25 kwa saa katika mchezo ambao Manchester United ilitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Newcastle United mwezi Januari.
Nafasi ya pili imeshikwa na Marcus Rashford.Rashford alikimbia kasi inayofikia 34.83 km/h katika mchezo dhidi ya Crystal Palace mwezi uliopita.
Aidha katika takwimu hizo mlinzi wa kushoto aliye majeruhi kwasasa Muingereza Luke Shaw ameingia mara mbili na anashika nafasi ya tatu.
Katika mchezo dhidi ya Swansea City,Shaw alitimua mbio kwa kazi ya 34.66 km/h na katika mchezo dhidi ya Tottenham uliochezwa Old Trafford alikimbia kwa kasi ya 34.59 km/h.
Nafasi ya nne imeshikwa na Mlinzi Chris Smalling.Katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa ugenini dhidi ya West Brom Smalling alikimbia kwa kasi ya 34.47
km/h.
0 comments:
Post a Comment