728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 29, 2016

    REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA 11 ULAYA,ATLETICO YAPOTEZA FAINALI YA TATU.

    MILAN,ITALIA.

    REAL MADRID wametwaa ubingwa wa Ulaya (Uefa Championships League) kwa mara ya 11 baada ya Jumamosi Usiku kuwachapa wapinzani wao Atletico Madrid kwa penati 5-3 kufuatia sare ya bao 1-1.

    Real Madrid ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi wake wa kati Sergio Ramos.Ramos alifunga bao hilo akimalizia mpira wa winga Gareth Bale.

    Mpaka mapumziko Real Madrid walikuwa mbele kwa bao hilo moja.Kipindi cha pili Atletico Madrid walikuja juu na kuwabana vizuri wapinzani na kufanikiwa kupata penati lakini Antonio Griezmann alipaisha.Penati hiyo ilipatakana baada ya Fernando Torres kuangushwa na Pepe kwenye boksi.Dakika ya 79 Atletico Madrid ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Yannick Ferreira-Carrasco.

    Carrasco aliyekuwa ameingia uwanjani akitokea benchi alifunga bao hilo akimalizia pasi ya mlinzi JuanFran na kufanya dakika 90 zimalizie matokeo yakibaki sare ya 1-1.Dakika 30 za nyongeza nazo hazikubadili matokeo.

    Ndipo mwamuzi Mark Clatterburg toka England alipoamuru ipigwe mikwaju ya penati ili kumpata mshindi na ndipo Real Madrid walipoibuka wababe kwa penati 5-3.

    Penati za Real Madrid zimefungwa na Lucas Vazquez, Marcelo,Gareth Bale Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo wakati zile za Atletico Madrid zikifungwa na Antonio Griezmann, Gabi na Saul Niguez.

    REKODI

    REAL MADRID imefanikiwa kutwaa ubingwa huo mara 11 katika historia huku Atletico Madrid wao wakiendelea kupoteza michezo ya fainali,sasa wamefikisha fainali tatu.

    Sergio Ramos amekuwa mlinzi wa kwanza kufikisha mabao mawili katika michezo ya fainali tangu michuano hiyo ilipofanyiwa marekebisho kutokuwa kuwa European Cup mpaka Uefa Champions League mwaka 1992


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA 11 ULAYA,ATLETICO YAPOTEZA FAINALI YA TATU. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top