Sunderland, England.
Marcus Rashford ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuifungia bao England katika mchezo wake wa kwanza (debut) wa kikosi cha wakubwa baada ya Ijumaa usiku kufunga bao moja na kuiwezesha England kutoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Australia katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa huko Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light.
Rashford akiwa na umri wa miaka 18 na siku 208 amefunga bao hilo dakika ya tatu tu ya machezo kwa mkwaju mkali akiunganisha krosi ya winga Raheem
Sterling na kumuacha mlinda mlango wa Australia Mathew Ryan akichupa bila mafanikio.
Bao jingine la England katika mchezo huo limefungwa na nahodha Wayne Rooney dakika ya 55 huku lile la Australia likipatikana baada ya kiungo wa England Erik Dier kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa.
Kufuatia bao hilo Rashford amefanikiwa kuivunja rekodi iliyowekwa Octoba,22,1938 na mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Everton,Chelsea na Arsenal Tommy Lawton.
Lawton akiwa na umri wa miaka 19 na siku 318 aliifungia England bao katika mchezo wake wa kwanza.Katika huo uliochezwa katika uwanja wa Ninian Park,England ilifungwa mabao 4–2 na ndugu zao Wales.
0 comments:
Post a Comment