728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 31, 2016

    KUELEKEA EURO 2016:UFARANSA YAICHAPA CAMEROON,SWEDENI BILA IBRAHIMOVIC HAKUNA KITU

    Nantes,Ufaransa.

    MKWAJU wa faulo wa dakika za majeruhi wa kiungo Dimitri Payet umeipa Ufaransa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Koloni lao la zamani Cameroon katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki wa kujipima nguvu uliochezwa katika uwanja wa Stade de la Beajouire jijini Nantes,Ufaransa.

    Wenyeji Ufaransa ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 20 tu ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Blaise Matuidi.Matuidi alifunga bao hilo kwa mkwaju mkali akiunganisha pasi ya kinda Kingsley Coman.

    Dakika mbili baadae yaani dakika ya 22 Cameroon walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake anayechezea FC Porto ya Ureno, Vincent Aboubakar.

    Dakika ya 41 mshambuliaji Olivier Giroud aliipa uongozi Ufaransa baada ya kufunga bao la pili akiunganisha krosi ya kiungo wa Juventus Paul Pogba na kufanya timu hizo ziende mapumziko matokeo yakiwa Ufaransa 2,Cameroon 1.

    Kipindi cha pili walikuwa ni Cameroon ambao walionekana hatari zaidi huku wakicheza kwa kujiamini na kuwabana vilivyo Wafaransa kiasi cha kumlazimisha kipa wao Hugo Lloris afanye kazi ya ziada kwa kuokoa michomo ya hatari.

    Lakini alikuwa ni Eric Maxim Choupo-Moting aliyefanikiwa kuunyamazisha uwanja wa Stade de la Beajouire baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 88 akitumia makosa ya mlinzi Laurent Koscielny aliyeshindwa kuondoa hatari golini kwake.

    Mchezo ukiwa unaelekea kuisha mkwaju mkali wa faulo wa uliopigwa na kiungo Dimitri Payet dakika ya 90 uliipatia Ufaransa bao la tatu na kufanye mpaka mwisho matokeo yawe 3-2.

    Ufaransa ambao ni wenyeji wa michuano ya Euro mwaka huu watarejea tena dimbani siku ya jumamosi kucheza mchezo wao wa mwisho wa kujipima nguvu pale watakaopovaana na Scotland huko Metz.

    Katika mchezo mwingine Swedeni wakiwa nyumbani Malmo bila ya nahodha wake Zlatan Ibrahimovic wamelazimishwa sare ya bila mabao na Slovenia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA EURO 2016:UFARANSA YAICHAPA CAMEROON,SWEDENI BILA IBRAHIMOVIC HAKUNA KITU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top