Accra,Ghana.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana,Yahaya Mohammed amekanusha vikali habari zilizoenea kuwa ametupiwa virago na klabu yake ya Azam FC yenye makao yake makuu Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.
Mohammed mwenye umri wa miaka 27 ameamua kuvunja ukimya baada ya juzi Alhamisi mtandao wa michezo wa nyumbani kwao Ghana wa GHANAsoccernet.com kuripoti ulifanya mahojiano na uongozi wa Azam FC na kuambiwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye rasta pamoja na mwenzake ambaye pia anatokea Ghana,Samuel Afful wameambiwa watafute vilabu vingine vya kuchezea msimu ujao.
Amesema "Sijaachwa na Azam FC.Viongozi hawajaniambia kitu kama hicho.
"Nimefanya mawasiliano na klabu na klabu haijafurahishwa kabisa na habari hizo".
"Bado nina mkataba na Azam FC na nina furaha kucheza soka Tanzania.Naamini msimu ujao utakuwa mzuri kwetu.
Mohammed alijiunga na Azam FC msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Aduana Stars aliyoifungia mabao 17 na kuiwezesha kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ghana.
0 comments:
Post a Comment