Minneapolis,Marekani.
MABAO mawili ya kipindi cha pili ya kiungo wa Brazil,Oscar Dos Santos,yameipa Chelsea ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AC Milan katika mchezo mkali wa kirafiki wa Michuano ya International Champions Cup (ICC) ulioisha hivi punde katika Uwanja wa U.S. Bank Stadium,ulioko Minneapolis,nchini Marekani.
Bertrand Traore aliiweka Chelsea mbele baada kufunga kwa kichwa dakika ya 24 ya mchezo lakini bao hilo halikudumu sana kwani dakika 38 Giacomo Bonaventura aliisawazishia AC Milan baada ya kufunga kwa mpira wa faulo.
Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na Kocha Antonio Conte ya kuwatoa Cesc Fabregas na Victor Moses na kuwaingiza Oscar Dos Santon na N'Golo Kante yaliipa uhai zaidi Chelsea ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Oscar dakika za 70 na 87.Bao la kwanza likiwa ni kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi mmoja wa AC Milan kunawa mpira ndani ya boksi.
Chelsea itashuka tena dimbani siku ya Jumapili kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki kwa kuvaana na Werder Bremen ya Ujerumani.
Vikosi
Chelsea (4-2-4): Courtois; Aina (Ivanovic 59), Terry (c), Cahill, Azpilicueta; Matic
(Chalobah 29), Fabregas (Oscar 59); Willian (Cuadrado 79), Traore (Hazard 52), Costa (Batshuayi 59), Moses (Kante 52).
AC Milan (4-3-3):Donnarumma; Abate
(Montolivo 60), Paletta, Romagnoli (Vergara 67), Calabria (Vido 81); Kucka,
Poli, Bonaventura; Suso (Zanellato 81), Luiz Adriano (Honda 67), Niang (Matri 81).
0 comments:
Post a Comment