London,England.
Timu ya Wanawake ya Arsenal jioni ya leo imetwaa ubingwa wa kombe la FA baada ya kuichapa timu ya Wanawake ya Chelsea kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Wembley jijini London.
Bao pekee la mchezo huo uliopigwa mbele ya watazamani 32,912 limefungwa dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na mshambuliaji kinda Danielle Carter.
Kabla ya kufunga bao hilo Carter,22 alimlamba chenga Hannah Blundell kabla ya kufumua mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa Chelsea Hedvig Lindahl na kutinga wavuni na kuifanya Arsenal itwae ubingwa wa 14 wa kombe hilo kongwe zaidi England.
0 comments:
Post a Comment