728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 08, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMATANO YA LEO JUNI 8,2016.

    Wilshere.

    Wilshere:Nyota wa zamani wa Manchester United, Gordon McQueen amemtaka kocha Jose Mourinho kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere,23, na kisha kuiunda timu kupitia kwa nyota huyo wa England.(Daily Mail)

    Vardy: Wachezaji waandamizi wa Leicester City,nahodha Wes Morgan,golikipa Kasper Schmeichel na mlinzi Robert Huth kwa pamoja wamemuomba 
    Mshambuliaji wa klabu hiyo Jamie Vardy,29, kuitosa ofa ya Arsenal na kubaki King Power.(Daily Telegraph)

    Ibrahimovic: Zlatan Ibrahimovic atachelewesha mpango wake wa kuhamia Manchester United mpaka hapo mwezi Julai ili aweze kupata bonasi ya uaminifu (loyalty bonus) ya £4m toka klabu yake ya sasa ya Paris Saint Germain.[ Telegraph]

    Nwakali:Arsenal inakaribia kutangaza kukamilisha usajili wa kiungo kinda wa Nigeria Kelechi Nwakali,18, kwa ada ya £3m kutoka katika shule ya soka ya 
    Diamond Football Academy.Nwakali ndiye aliyekiongoza kikosi cha U17 cha Nigeria kutwaa kombe la dunia la vijana mwaka Jana na kiuchezaji amekuwa akifananishwa na kiungo wa Manchester City Muivory Coast Yaya Toure.(Mirror)

    Klopp:Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amesema uwepo kwake katika michuano ya kombe la Copa America huko Marekani hasa katika mchezo wa Jumanne kati ya Argentina na Chile haimaanishi kuwa alikwenda kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain bali alikwenda mapumzikoni tu.(Liverpool Echo)

    Matic:Kiungo mahiri wa Chelsea Nemanja Matic amemwambia Kocha mkuu wa klabu hiyo  Antonio Conte kuwa anataka kuhamia Manchester United ili kuungana na kocha wake wa zamani Mreno Jose Mourinho.(The Sun)

    Aubameyang:Manchester City imeripotiwa kuwa tayari kutoa £50m ili kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.Hatua hiyo imekuja baada ya vilabu hivyo wiwili kuanza mazungumzo rasmi siku ya Jumanne.(Daily Mirror)

    Rodriguez:Paris Saint-Germain imeripotiwa kufanya mawasiliano na Real Madrid ili kuangalia uwezekano wa kumsajili staa wake Mcolombia James Rogriguez,23, kwa kitita cha €90m.(AS)

    Mane:Liverpool inaandaa kitita cha £30 kwa ajili ya kumsajili winga wa Southampton Msenegal Sadio Mane.Kocha Jurgen Klopp anamuona Mane,23,kuwa mtu sahihi wa kukiongezea makali kikosi hicho tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England.(The Sun)

    Skrtel:Middlesbrough imeachana na mpango wa kutaka kumsajili mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel na badala yake mlinzi huyo mwenye miaka 31ataelekea Uturuki kujiunga na mabingwa wa nchi hiyo Besiktas.(Express)

    Bellerin:Baada ya kusikia kuwa mlinzi wake wa kulia Muhispania Hector Bellerin anawindwa na Barcelona, Arsenal imeripotiwa kuanza mchakato kabambe wa kumsainisha mkataba mpya wa muda mrefu nyota huyo mwenye miaka 21.(The Sun)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMATANO YA LEO JUNI 8,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top