Manchester, England.
Hatimaye Manchester United leo imekamilisha usajili wa mlinzi wa Ivory Coast Eric Bailly kutoka Villarreal ya Hispania kwa ada ya uhamisho ya € 32m.
Bailly, 22,amesaini mkataba wa miaka minne wenye kipengele cha kurefushwa kwa miaka miwili zaidi.
Bailly anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Manchester United tangu miamba hiyo ya Old Trafford impe kibarua kocha Mreno Jose Mourinho wiki moja iliyopita.
Bailly ameichezea Villarreal michezo 47 tangu alipojiunga nayo miezi 16 iliyopita akitokea Espanyol.Ameichezea Ivory Coast michezo 15 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment