728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 08, 2016

    COUTINHO WA YANGA AJIPELEKA SIMBA,ASEMA AMEIMISS TANZANIA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    UNAMKUMBUKA yule Mbrazil wa zamani wa Yanga anayeitwa Andrey Coutinho? Ni hivi,wakati Wanajangwani hao wakimtimua kwa madai ya kutoridhishwa na kiwango chake anauwasha moto huko kwao na amewaita Simba wakazungumze.

    Kiungo huyo ambaye mashabiki wengi wa Yanga walikuwa wakimpenda kutokana na mbwembwe zake za kuhamasisha awapo ndani ya uwanja, kwa sasa anaichezea klabu
    ya Myanmar ambapo katika michezo 11 aliyocheza anasema amefanikiwa kufunga mabao saba.

    Akizungumza Jumatano kwa njia ya mtandao, alisema anaikumbuka sana
    Tanzania kutokana na ukarimu wao na kutamka wazi kuwa angependa kuja tena kucheza timu yoyote hata ikiwa Simba.

    “Kwa ujumla nimepamis sana Tanzania,nimewamis mashabiki pia, kwasasa naichezea timu ya Myanmar na katika michezo yangu 11 ambayo nimecheza nifanikiwa kufunga mabao saba, najitahidi sana kuzidi kuboresha kiwango changu,” alisema.

    Dimba lilipomuuliza kama yupo tayari kuchezea Simba alijibu: “Mkataba wangu na Myanmar, unamalizika Agosti mwaka huu hivyo kama watakuwa tayari kuzungumza na mimi hakuna shida kwani napapenda sana Tanzania,” alisema.

    Akizungumzia hatua waliyofikia Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kutinga hatua ya makundi alisema ana imani kubwa kwamba watafika mbali zaidi kama watazidi kushikamana.

    CHANZO:DIMBA

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COUTINHO WA YANGA AJIPELEKA SIMBA,ASEMA AMEIMISS TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top