728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 14, 2016

    SUAREZ AIPA FC BARCELONA UBINGWA WA 24 WA LA LIGA,ATWAA TUZO YA PICHICHI

    Barcelona,Hispania.

    Mabao matatu ya Mruguayi Luis Suarez yameiwezesha FC Barcelona kutwaa ubingwa wa 24 wa Ligi daraja la Kwanza Hispania maarufu kama La Liga baada ya jioni hii kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Granada katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliopigwa kwenye dimba la Estadio Nuevo Los Carmenes.

    Suarez amefunga mabao hayo matatu dakika za 22,38 na 86 kwa pasi za Dani Alves,Jordi Alba na Neymar Dos Santos na kutwaa tuzo ya PICHICHI (ufungaji bora wa La Liga) baada ya kufikisha mabao 40.Jumla akifikisha mabao 59katika michuano yote.

    Katika mchezo mwingine wa La Liga Real Madrid imeichapa Deportivo La Coruna kwa mabao 2-0 mabao yote yamefungwa na Mreno Cristiano Ronaldo na kumfanya afikishe mabao 35 La Liga.Jumla 51

    REKODI

    Suarez amekuwa mchezaji wa kwanza mbali ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuweza kuibuka mfungaji bora wa La Liga tangu mwaka 2008–09,Mruguayi Diego Forlan alipoibuka kinara baada ya kufunga mabao 32 akiwa na Atletico Madrid.

    Ubingwa wa leo pia ni wa sita kwa FC Barcelona kutwaa tarehe kama ya leo yaani Mei 14 mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni mwaka 2005.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SUAREZ AIPA FC BARCELONA UBINGWA WA 24 WA LA LIGA,ATWAA TUZO YA PICHICHI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top