728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 14, 2016

    VPL:YANGA,NDANDA HAKUNA MBABE

    Dar es salaam,Tanzania.

    Ndanda FC na Yanga SC zimeshindwa kutambiana baada ya leo jioni kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom Uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.

    Wenyeji Ndanda FC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 29 ya mchezo kupitia kwa Omar Mponda.Mponda alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Atupele Green kuangushwa ndani ya box na Juma Abdul.

    Yanga ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 35 kupitia kwa winga Simon Msuva.Msuva alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Geoffrey Mwashiuya.

    Dakika ya 41 Yanga ilipata bao la pili kupitia kwa Donald Ngoma.Ngoma alifunga bao hilo akimalizia mkwaju wa mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi Mgwali

    Salum Minely aliisawazishia Ndanda FC bao dakika ya 79 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Omary Mponda na kufanya matokeo yawe sare ya mabao 2-2.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:YANGA,NDANDA HAKUNA MBABE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top