728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 14, 2016

    HIZI HAPA HABARI 14 ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAMOSI YA LEO MEI 16/2016


    Na sokaextra.blogspot.com

    Slimani:Leicester City imeiambia Sporting Lisbon kuwa iko tayari kufikia dau la €30m (£23.6m) kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu hiyo Mualgeria Islam Slimani,27.Msimu huu Slimani amefunga mabao 30 katika michezo 42.(A Bola)

    Osvaldo:Mshambuliaji wa zamani wa Southampton Dani Osvaldo ametupiwa virago na klabu yake ya Boca Juniors baada ya kubishana na kocha wa klabu hiyo Guillermo Barros Schelotto kufuatia kufumwa chooni akivuta sigara.(Goal.com)

    Bolt:Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Mjamaica Usain Bolt,24 ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester United amesema siku moja angependa kuichezea timu hiyo lakini si chini ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Mholanzi Louis van Gaal.(Daily Mirror)

    Xhaka:Kiungo wa Borussia Monchengladbach Mswisi Granit Xhaka,24 anataka kuona suala lake la kuhamia Arsenal linakamilika kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016 hii ni baada ya Arsenal kudaiwa kutuma ofa ya £34m.(Daily Star)

    Arsenal:Arsenal imeripotiwa kuandaa kitita cha £54m pekee cha kufanyia usajili licha ya kudaiwa kuwa na fedha nyingi benki.(Evening Standard)

    Mario:PSG imetuma ofa rasmi ya €35m kwenda Sporting Clube de Lisbon kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu hiyo João Mario ambaye pia anawindwa na Manchester United.Sporting imemthaminisha Mario kuwa na thamani ya €60.(France Football)

    De Boer:Everton imefungia mazungumzo na kocha wa zamani wa Ajax Mholanzi Frank de Boer ili aweze kukinoa kikosi hicho msimu ujao. (Daily Mail)

    Mazzarri:Kocha wa zamani wa Inter Milan Walter Mazzarri anawindwa na Watford ili aje kuchukua nafasi ya Quique Sanchez
    Flores anayeondoka.(Watford Observer).

    Janmaat:Mlinzi Daryl Janmaat huenda akawa mchezaji wa kwanza kuikimbia Newcastle United baada ya kuripotiwa kuanza kufukuziwa na Juventus ya Italia.(Newcastle Chronicle)

    Arteta:Kiungo wa Arsenal Mikel Arteta anakaribia kufikia makubaliano ya kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Manchester City baada ya kupendekezwa na kocha wake mpya Pep Guardiola. (Manchester Evening News)

    Allardyce:Kocha wa Sunderland Sam Allardyce anataka kukiongezea nguvu kikosi chake kwa kuwasajili winga wa Swansea City Andre Ayew na mlinzi wa Lorient Lamine Gassama.(Daily Mirror)

    Martial:PSG imeripotiwa kukutana na wawakilishi wa nyota wa Manchester United Mfaransa Antony Martial kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 17 msimu huu.(L'Equipe)

    Karius:Liverpool imeripotiwa kuwa karibu kumsajili kipa wa Mainz Loris Karius.Taarifa nyingine zinadai nyota huyo mwenye miaka 22 atasubiri kwanza kuona kama Liverpool itapata nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.(Bild)

    Rashford:Kocha wa England Roy Hodgson atamuongea kikosini mshambuliaji mkongwe wa Sunderland Jermain Defoe tayari kwa michuano ijayo ya Euro.Wakati huohuo kinda wa Manchester United Marcus Rashford amepata mwaliko wa kufanya mazoezi na kikosi cha England kitakachoanza kambi kwa ajili ya michuano ya Euro.(Daily Mirror)




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI 14 ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAMOSI YA LEO MEI 16/2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top