728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 14, 2016

    HAMIS KIIZA KUACHANA NA SIMBA,ATOA SABABU MBILI KUBWA

    Dar es salaam,Tanzania.

    KINARA wa mabao wa Simba,Hamisi Kiiza, amesema anaweza kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika kwa sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya viongozi wa timu hiyo kutokuwa na imani naye pamoja na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

    Mganda huyo amejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu na ametoa mchango mkubwa kwa timu yake ikiwemo kuifungia mabao 19 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

    Mshambuliaji huyo alisema jitihada zake zote alizokuwa akizitoa kwa Simba ipate kushiriki michuano ya kimataifa, ambayo ingemsaidia kuonekana ili kuendelea na safari yake ya kucheza soka la kimataifa zimekuwa kinyume hivyo ataangalia
    kama ataweza kubaki.

    “Bado nina mkataba wa mwaka mmoja Simba, lakini ukweli msimu umekuwa mbaya hasa kipindi cha mwishoni, yapo mengi yameongewa dhidi yangu kuwa mtovu wa nidhamu, lakini pia sijafurahishwa na timu kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, hicho kinaweza kunifanya niondoke“alisema Kiiza.

    Mganda huyo ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga, alisema bado hajajua wapi pa kwenda, lakini kwa uwezo aliokuwa nao anaamini hawezi kukosa timu iwe Tanzania,Kenya au nyumbani kwao Uganda.

    Alisema kitu kingine kinachomfanya atake kuondoka Simba ni baadhi ya viongozi na wanachama wa timu hiyo kumshutumu kuwa yeye ana mapenzi na Yanga, kwa sababu alishindwa kuifunga katika mechi mbili ambazo walikutana msimu huu.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HAMIS KIIZA KUACHANA NA SIMBA,ATOA SABABU MBILI KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top