Barcelona,Hispania.
Barcelona ndiyo klabu iliyouza jezi nyingi zaidi duniani kwa msimu wa mwaka 2015/16.
Kwa mujibu wa takwimu za mwezi Aprili,Barcelona inayochezewa na mchezaji bora duniani kwa sasa Muargentina Lionel Messi imefanikiwa kuuza jumla ya jezi halali milioni 3.637 duniani kote.
Kwa vilabu toka Ligi Kuu England Chelsea imeshika nafasi ya kwanza baada ya kufanikiwa kuuza jumla ya jezi 3,102,000,duniani iko nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona na Bayern Munich.
Manchester United ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikitamba katika mauzo msimu huu imeshuka mpaka nafasi ya nne kidunia,England nafasi ya pili.Real Madrid iko nafasi ya tano ikiwa imefanikiwa kupandisha mauzo yake kwa asilimia 11 pekee toka katika mauzo yake ya msimu uliopita.
Arsenal iko nafasi ya tatu kwa England,nafasi ya saba kidunia nyuma ya Paris Saint-Germain inayoshikilia nafasi ya sita.
AC Milan na Juventus ndiyo vilabu pekee kutoka Italia vilivyofanikiwa kujipenyeza katika nafasi kumi za juu.Vinashika nafasi ya tisa na kumi.
Klabu na Idadi ya jezi ilizouza kufikia Aprili kwa msimu wa 2015/2016.
1 FC Barcelona 3.637 million
2 Bayern Munich 3.312 million
3 Chelsea 3.102 million
4 Manchester
United 2.977 million
5 Real Madrid 2.866 million
6 Paris Saint-
Germain 2.212 million
7 Arsenal 2.055 million
8 Atletico Madrid 1.977 million
9 Juventus 1.678 million
10 AC Milan 1.287 millionhj
0 comments:
Post a Comment