728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 01, 2015

    REKODI:RONALDO AFIKISHA MAGOLI 501,AIFIKIA REKODI YA RAUL,FAHAMU MENGI KUHUSU MAGOLI HAYO HAPA

    Madrid,Madrid.

    MFALME.Cristiano Ronaldo ameendelea kujichimbia katika vitabu vya kumbukumbu vya Real Madrid baada ya hapo jana jumatano usiku kuifungia klabu hiyo magoli mawili katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Malmo FF ya Sweden na kufanikiwa kufikisha jumla ya magoli 501 katika maisha yake ya soka.

    Magoli hayo 501 yamekuja baada ya jumla ya michezo 753.Magoli 323 akiwa na Real Madrid,118 akiwa na Manchester United,5 akiwa na Sporting Lisbon na 55 akiwa na Ureno.

    Aifikia rekodi ya Raul Gonzalez

    Magoli mawili dhidi ya Malmo FF siyo kwamba yamemfanya Ronaldo awe ameifungia Real Madrid magoli 82 katika ligi ya mabingwa bali pia yamemfanya afikishe magoli 323 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya Hispania sawa na mzawa Raul Gonzalez Blanco.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REKODI:RONALDO AFIKISHA MAGOLI 501,AIFIKIA REKODI YA RAUL,FAHAMU MENGI KUHUSU MAGOLI HAYO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top