London,England.
Goli la kusawazisha la dakika ya 37 la kiungo Emre Can limeiokoa Liverpool isikumbane na kipigo toka kwa wageni Rubin Kazan katika mchezo wa kundi B wa michuano ya Europa Ligi ulipigwa jana usiku katika dimba la Anfield,Liverpool.
Liverpool ambayo ilikuwa inacheza mchezo wake wa kwanza nyumbani ikiwa chini ya kocha mpya Jurgen Klopp ilijikuta ikiwa nyuma baada ya Marko Devic kuifungia Kazan dakika ya 15.
Kuingia kwa goli hilo kuliiamsha Liverpool na kufanikiwa kupata goli hilo la kusawazisha kupitia kwa Can.Michezo ya marudiano ya Europa Ligi itapigwa Novemba 8.
Kwingine katika dimba la Constant Vanden Stock huko Blussels, Tottenham ilijikuta ikipokea kipigo cha magoli 2-1 toka kwa Anderletch ya Ubelgiji licha ya kuwa mbele kwa kwa goli la mapema la kiungo Christian Eriksen. Anderletch ilipata magoli hayo dakika za 13 na 75 kupitia kwa Guillaume Gillet na Stefano Okaka Chuka.
Matokeo mengine ni kama ifuatavyo....
Fenerbahçe 1-0 Ajax
Molde 3-1 Celtic
Bordeaux 0-1 FC Sion
Liverpool 1-1 Rubin Kazan
FK Qabala 1-3 Bor Dortmd
PAOK Salonika 0-0 FK Krasnodar
FC Midtjylland 1-4 Napoli
Legia Warsaw 1-1 Club Brugge
SK Rapid Vienna 3-2 Viktoria Plzen
Villarreal 4-0 Dinamo Minsk
Slovan Liberec 1-1 FC Groningen
Sporting Braga 3-2 Marseille
Dnipro Dnipropetrovsk 0-1 St Etienne
Lazio 3-1 Rosenborg
Lokomotiv Moscow 1-1 Besiktas
Sporting 5-1 Skenderbeu Korce
FC Basel 1-2 Belenenses
Fiorentina 1-2 Lech Poznan
Monaco 1-0 FK Qarabag
Anderlecht 2-1 Tottenham
Apoel Nic 2-1 Asteras Tripolis
Schalke 2-2 Sparta Prague
AZ Alkmaar 0-1 FC Augsburg
Partizan Belgrade 0-2 Ath Bilbao
0 comments:
Post a Comment