728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 24, 2015

    SAKATA LA KUKUTWA NA HIRIZI "POWER BANK":MSENEGAL WA SIMBA ASEMA HAJUI CHOCHOTE WALA HAUSIKI

    Unaweza kuona kama miujiza! Straika wa Simba, Pape N’daw, amekana kukutwa na hirizi na amesema hajawahi kujihusisha na vitendo vya kishirikina na hata siku moja hawezi kushiriki vitendo hivyo.

    Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya akicheza dhidi ya Prisons, N’daw, raia wa Senegal, alizongwa na wachezaji wa timu ya Prisons kisha akakutwa na hirizi ambapo mwamuzi alimtoa nje kwenda kuitoa.

    N’daw amesema: “Sikukutwa na kitu chochote, ndiyo maana nilikuwa nabishana na wale wachezaji, kama kuna kitu kimeonekana hakinihusu mimi.”

    Kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya ushirikina uwanjani straika wa Simba, Pape N’daw yupo hatarini kupewa adhabu y kufungiwa kucheza mechi zisizopungu tatu za Ligi Kuu Bara.

    Pia, kwa mujibu wa kanuni na 37 ya ligi kuu kipengele cha (e), N’daw atafungiwa kucheza mechi tatu na kupigwa faini y Sh 500,000 kwa kosa hilo.

    Kanuni hiyo inasema kuwa kufanya vitendo vyenye kuonye imani za kishirikina, uchawi adhabu yake itakuwa ni kufung mechi tatu na faini ya Sh laki tano.

    (Chanzo:Saleh Jembe Blog)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAKATA LA KUKUTWA NA HIRIZI "POWER BANK":MSENEGAL WA SIMBA ASEMA HAJUI CHOCHOTE WALA HAUSIKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top