728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 14, 2015

    MASHABIKI BAYERN WAPANGA KUGOMEA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA DHIDI YA ARSENAL

    Munich,Ujerumani.

    Kikundi cha mashabiki wa Bayern Munich "FC Bayern Worldwide" kinapanga kugomea kwa dakika 5 mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Arsenal kwa kile kinachosemekana kuwa ni ukubwa wa kiingilio katika uwanja wa Emirates.

    Bayern Munich na Arsenal zinatarajia kumenyana Octoba 20 katika uwanja wa Emirates tukio ambalo litawalazimu mashabiki kutoka Ujerumani kutoa kati ya £64 na £74 kama kiingilio katika mchezo huo.

    Mashabiki hao wanaona kiingilio hicho ni kikubwa mno na hivyo wamepanga kufanya mgomo wa dakika hizo 5 kwa kubaki nje ya uwanja huku mchezo ukiendelea ili kuvionyesha vilabu na vyama vya soka jinsi soka linavyokuwa bila ya mashabiki na kisha kutumia dakika 85 ndani ya uwanja kuonyesha jinsi soka linavyokuwa pindi linapokuwa na mashabiki.

    Hii ni mara ya pili kwa mashabiki wa Bayern Munich kulalamikia kiingilia katika uwanja uwanja wa Emirates,mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 ambapo ilibidi kiingilio kipunguzwe kutoka £64 mpaka £37. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MASHABIKI BAYERN WAPANGA KUGOMEA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA DHIDI YA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top