BILIONEA maarufu nchini na mdau wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘MO’, ametoa fedha kwa klabu hiyo kwa ajili ya kuhakikisha straika hatari wa Vital’O ya Burundi anatua Msimbazi haraka iwezekanavyo.
MO amechukua uamuzi huo ilikukiimarisha kikosi cha Simba ambacho msimu huu kinaonekana kukosa makali kutokana na kumtegemea zaidi straika mmoja tu ambaye ni Hamis Kiiza na timu imekuwa ikipata wakati mgumu pale staa huyo anapokosekana.
Mavugo, ambaye ni mmoja kati ya mastraika hatari sana nchini Burundi, ambapo msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa ligi ya nchi hiyo, akifunga mabao 30 katika mechi 31, amekuwa akifukuziwa na Simba kwa muda sasa, kitu ambacho kimlazimisha MO kuingilia kati usajili wake ili amlete kusaidiana na Kiiza na watengeneze safu kali zaidi ya ushambuliaji.
Habari za uhakika zinadai kuwa MO ameahidi kutoa dola 50,000 (Sh milioni 106.9) ili kufanikisha ujio wa Mavugo,ambaye alishindwa kutua Msimbazi wakati wa usajili wa dirisha kubwa kutokana na klabu yake ya Vital’O kupandisha bei yake.
Chanzo cha habari kilisema kuwa Simba imekuwa ikimtolea macho Mavugo kwamuda mrefu, lakini walishindwa kumsajili baada ya klabu yake kupandisha dau la usajili, ndiyo maana sasa hivi MO ameamua kutoa fedha kuhakikisha straika huyo anatua Simba.
“Mavugo alikuwa chaguo letu la kwanza, lakini tuliachana naye baada ya klabu yake ya Vital’O kuingia tamaa na kupandisha dau katika dakika za mwisho.” Kilisema chanzo hicho.“Kuona hivyo tuliachana naye, lakini sasa MO ameahidi kutoa fedha ili kuisaidia Simba kumnasa huyu jamaa.”

Chanzo:Gazeti la BINGWA Leo.
0 comments:
Post a Comment