Mechi za raundi ya 11 za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zichezwe
Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika Desemba 12 na 13 kupisha
maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inatarajia kuingia kambini mapema mwezi ujao kujiandaa na
mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo itafanyika Novemba 14 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana nchini
Algeria, Novemba 17 mwaka huu.
Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni kati ya Mgambo
Shooting na Yanga (Tanga), Kagera Sugar na Ndanda (Tabora), Stand United
na Mwadui (Shinyanga), Mbeya City na Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam na
Simba (Dar es Salaam) na Majimaji na Toto Africans (Songea). Mechi za
Desemba 13 ni kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons (Dar es Salaam), na
Coastal Union na African Sports (Tanga).
Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa Oktoba 4 mwaka
huu kupisha mechi ya Taifa Stars na Malawi sasa zitafanyika Desemba 16
mwaka huu. Mechi hizo ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam),
na African Sports na Yanga (Tanga), mchezo kati ya Ndanda na Simba
(Mtwara utapangiwa tarehe ya kuchezwa.
Nayo mechi namba 59 kati ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar iliyokuwa
ichezwe Oktoba 21 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam imesogezwa
mbele kwa siku moja hadi Oktoba 22 mwaka huu ili kuipa nafasi ya
mapumziko JKT Ruvu ambayo jana (Oktoba 18 mwaka huu) ilicheza mechi yake
ya raundi saba mkoani Shinyanga
0 comments:
Post a Comment