Nyota wa Arsenal Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain watakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu kila mmoja baada ya kupata majeraha katika mchezo wa kombe la ligi "Capital One" katika mchezo ambao Arsenal ililala kwa bao 3-0 toka kwa Sheffield Wednesday jumanne usiku.
Kufuatia majeraha hayo nyota hao watakosa michezo mitatu muhimu ya klabu hiyo.Michezo hiyo ni dhidi ya Swansea City,Bayern Munich na Tottenham pamoja na michezo ya kimataifa ya kirafiki ya timu ya taifa ya England ambayo inatarajiwa kupimana nguvu na Hispania kisha Ufaransa baadae mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment