728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 24, 2015

    MANCHESTER CITY YAJIPANGA KUIPIGA BAO ARSENAL KWA KUMSAJILI NDUGU WA ROBERT LEWANDOWSKI

    Manchester,England.

    Manchester City inajiandaa kuipiga bao Arsenal kwa kumsajili kiungo wa Sevilla na timu ya taifa ya Poland Grzegorz Krychowiak.

    Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita Krychowiak,25 amekuwa akiwindwa na Arsenal ili kuja kuimarisha safu yake ya kiungo cha ulinzi ambayo kwa kipindi kirefu ilikuwa ikimtegemea Mikel Arteta kabla ya kuibuka kwa Francis Coquelin lakini mpango ulikuja kukwama katika majira ya joto yaliyopita baada ya Arsenal kukataa kutoa kitita cha €30m (£22m) kwa madai kuwa kiwango hicho ni kikubwa mno.

    Sasa baada ya Arsenal kudegua Manchester City imeripotiwa kuwa tayari kuvunja benki kumnasa kiungo huyo baada ya kiungo Yaya Toure hivi karibuni kudai kuwa hana furaha klabuni hapo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAJIPANGA KUIPIGA BAO ARSENAL KWA KUMSAJILI NDUGU WA ROBERT LEWANDOWSKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top