Mshambuliaji aliyekatika kiwango cha juu hivi sasa duniani Pierre-Emerick Aubameyang amefichua kwamba ana ndoto ya kucheza ligi ya Hispania La Liga hapo baadae ikiwa ataona ametosheka kukipiga Borussia Dortmund.
Pierre-Emerick Aubameyang,26 raia wa Gabon ndiye kinara wa mabao kwa sasa katika ligi ya Bundesliga baada ya kufunga mabao 13 katika michezo 10 huku akifuatiwa kwa karibu na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.
Aubemeyang ambaye ana mkataba na Borussia Dortmund mpaka 2020,amesema angependa kujipima kwa kucheza Hispania alikozaliwa mama yake mzazi.
"Siku moja nitaondoka na kutua ligi nyingine,"Aubameyang aliiambia BBC World Service. "Ndoto yangu ni kucheza Hispania.
"Watu wengi wanaona kuwa England kunanifaa zaidi,mama yangu ni Muhispania,ningependa kucheza hapo kwanza kisha England baadae ikibidi
0 comments:
Post a Comment