728x90 AdSpace

Monday, October 12, 2015

FERGUSON AFUNGUKA SABABU ILIYOFANYA ASHINDWE KUMSAJILI DAVID SILVA


Alex Ferguson ana mambo,kitabu chake kipya kiitwacho  Leading pia kina mambo.Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametoa sababu iliyofanya ashindwe kumsajili kiungo wa Manchester City,David Silva licha ya kuwa ni moja kati ya viungo wazuri sana duniani.

Ferguson akiwa katika harakati za kukinadi (promotion) kitabu chake kipya huko New York amesema hakumsajili Silva kwa sababu kiungo huyo siyo mzuri katika kukaba. 
Amesema"Tulimfuatilia mara nyingi Silva wakati akiwa Valencia lakini tukagundua hana msaada wakati timu haina mpira,siyo mkabaji.Wakati umri ulipoanza kunitupa mkono niliacha kucheza kama mshambuliaji namba 9 nikarudi kucheza namba 10 hivyo najua kile ambacho nilitaka namba 10 wangu awe.Nilitaka mtu mwenye uwezo wa kusaidia ulinzi wakati timu inaposhambulia kitu ambacho Silva hakuwa nacho".

Silva alijiunga na Manchester City mwaka 2010 kwa ada ya  £24m akitokea Valencia ya Hispania.Mpaka sasa Silva ameisaidia Manchester City kutwaa mataji mawili ya ligi kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: FERGUSON AFUNGUKA SABABU ILIYOFANYA ASHINDWE KUMSAJILI DAVID SILVA Rating: 5 Reviewed By: Unknown