Kutoka Daily Mirror jumapili ya leo habari zinasema Chelsea inafikiria kumuajiri Diego Simeone ikiwa itaamua kuachana na Jose Mourinho.
Habari zinazidi kupasha kuwa viongozi wa juu wa klabu hiyo tayari wameshaanza kulifanyia kazi jambo hilo lakini kikwazo kikubwa kimeripotiwa kuwa ni dau la £15m ambalo Atletico Madrid italitaka ili kumuachia kocha huyo raia wa Argentina ambaye bado ana mkataba mrefu katika klabu hiyo ya Vicente Cardelon.
0 comments:
Post a Comment