Sunderland imemtangaza Sam Allardyce kuwa kocha wake mpya baada ya kuachana na Dick Advocaat.
Allardyce,60 amesaini mkataba wa miaka miwili leo hii na kuahidi kuipatia mafanikio klabu hiyo kongwe ya ligi kuu England.
Allardyce anarejea Sunderland kwa mara ya tatu baada ya kuichezea miaka ya 1980's na kurejea tena 1996 akiwa kama kocha wa kikosi cha vijana.
Sunderland inakuwa ni klabu ya sita kufundishwa na Allardyce baada ya Bolton Wanderers, Newcastle United, Blackburn Rovers na West Ham United.
Aandika historia Wear - Tyne
Sam Allardyce anakuwa ni kocha wa kwanza kuvifundisha vilabu hasimu vya Sunderland na Newcastle United vinavyotokea katika mji wa Sunderland na mchezo wao huitwa Wear - Tyne Derby.
0 comments:
Post a Comment