Paris,Ufaransa.
Luis Suarez akiwatoka walinzi wa PSG ya Ufaransa
Barcelona imepewa ofa ya kucheza ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue na shabiki wake mkubwa –Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ikiwa itazuiwa kushiriki ligi ya La Liga kufuatia jimbo la Catalunya kutaka kujiondoa Hispania na kuwa taifa huru.
Ofa hiyo ya Valls imekuja baada ya katibu mkuu wa La Liga Javier Tebas kutanabaisha kwamba Barcalona itaondolewa katika orodha ya vilabu vya La Liga ikiwa jimbo la Catalunya litafanikiwa kujiondoa katika milki ya Hispania.
'Kama Catalunya itakuwa huru,ukizingatia na sheria zitakazopitishwa na vilabu vingine vya Hispania, Barcelona hataruhusiwa kuwemo La Liga," Alisema Tebas.
"Monaco inacheza Ligue One,kwanini ishindikane kwa Barcelona?Mimi ni shabiki mkubwa wa mpira,shabiki wa Barcelona,”Valls aliliambia gazeti la siasa la nchi hiyo Challenges.
“Barcelona iko katika damu yangu.Wafaransa wanalijua hilo na wamekuwa wakiniuliza maswahili mengi mtaani kuhusu hali ya Catalunya na majaaliwa ya Barcelona."
0 comments:
Post a Comment