Makinda Marc Bola na Glen Kamara wakigombea mpira mazoezini
London,England.
Kocha mkuu wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amewaita makinda 13 katika kikosi chake kitakachoivaa Sheffield Wednesday FC leo usiku katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya kombe la Capital One utakaopigwa katika dimba la Hillsborough.
Makinda walioitwa toka kikosi cha vijana cha klabu hiyo ni Alex Iwobi, Ben Sheaf, Marcus Agyei-Tabi, Donyell Malen, Joshua Dasilva, Reiss Nelson, Ismael Bennacer, Savvas Mourgos, Glen Kamara, Matt Macey, Marc Bola, Krystian Bielik na Julio Pleguezuelo.
Mbali ya makinda hao pia Wenger amepanga kuwapa nafasi wachezaji wasiokuwa na nafasi kikosi cha kwanza ili kuonyesha uwezo wao.Nyota hao ni Joel Campbell,Calum Chambers,Keylan Gibbs na Mathew Flamini huku nyota kama Olivier Giroud,Alexis Sanchez,Mesut Ozil,Santiago Cazorla wakipumzishwa kwa ajili ya kuivaa Swansea City wikendi ijayo kisha Bayern Munich siku chache baadae katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa.
Vikosi huenda vikawa hivi
0 comments:
Post a Comment