728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 19, 2015

    ETIHAD YAKANA KUKARIBIA KUIDHAMINI INTER MILAN

    Milan,Italia.

    Kampuni ya usafiri wa ndege ya Etihad yenye makazi yake huko Abu Dhabi,Dubai imekana kuwa katika mazungumzo ya kutaka kuidhamini Inter Milan kwa kitita cha €125m.

    Mapema wiki iliyopita taarifa kutoka vyombo vya habari vya Italia ziliripoti kuwa Inter Milan iko karibu kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Etihad utakaoiwezesha miamba hiyo ya Seria A kuvuna kitita cha €25m kwa mwaka ambacho ni €13m zaidi ya kile wanachokipata kwa sasa toka kampuni ya kutengeneza matairi ya Pirelli.

    Pireli imeidhamini Inter Milan kwa kipindi cha miaka 20 sasa na mkataba huo unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu huu wa ligi ya Seria A.

    Sassuolo ndiyo klabu yenye udhamini mkubwa Italia ikidhaminiwa na Mapei kwa kitita cha €22m ikifuatiwa na vilabu vya Juventus na AC Milan ambavyo kila kikoja kina udhamini wa €17m kutoka Jeep na Emirates. 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ETIHAD YAKANA KUKARIBIA KUIDHAMINI INTER MILAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top